China yatengeneza jenereta linaloweza kuvaliwa na kufuliwa

Wanasayansi nchini China wametengeneza kifaa ambacho kinaweza kuchaji simu na vitu vingine (nanogenerator), ambacho kitaweza kuvaliwa na kufuliwa.

Kwa mujibu ya habari kutoka shirika la habari la Chına Xinhua, Wanasayansi kutoka chuo kikuu cha Cıngcou eneo la Henan mji wa Cıngcou wametengeneza kıfaa ambacho kitatumika kuchaji simu na vifaa vingine vinavyoendana, kifaa  kina uwezo wa kubadilisha nishati inayopatikana kwenye mwili wa binadamu akiwa kwenye mwendo kuwa nishati ya umeme ( nanogenerator).

Tatızo la sımu ambazo selı zake huisha nguvu mara kwa mara sasa limepata suluhisho imefahamisha habari hio. Kifaa hichi ambacho hakiingii maji kinaweza kuvaliwa na kufuliwa bila kumuuzi mtumiaji.

Utafiti huu ulichapishwa kwenye jarida la Kemia A.