https://monetag.com/?ref_id=TTIb DC Muro atoa onyo kwa vyama vya siasa kuacha malumbano | Muungwana BLOG

DC Muro atoa onyo kwa vyama vya siasa kuacha malumbano


Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro amevitaka vyama vya siasa kuacha  malumbano na mvutano isiyokuwa na tija kwa wananchi wa Arumeru na badala yake amewataka kuungana na serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Arumeru.

Muro ameyasema hayo baada ya kuingilia kati mgogoro wa umiliki wa jengo ambalo awali lilikuwa likitumiwa na chama cha ushirika kata ya Ilikiurei hatua iliyosababisha kufungwa kwa ofisi ya serikali ambayo ilikuwa ikihudumia wananchi wa vitongoji viwili.

Kwa upande wao wananchi wanaoishi katika vitongoji hivyo mbali na kumpongeza DC Muro kwa kuchukua hatua kwa haraka kuwa ofisi hizo zifunguliwe wamesema uamuzi huo utawasaidia kupata huduma ambazo wamekuwa wakizikosa kwa muda mrefu kutokana na mvutano wa umiliki wa jengo hilo kutoka kwenye vyama viwili vya siasa.