Jackline Wolper amvaa Esha Buheti kisa Wema Sepetu

 Bado Wema Sepetu anazidi kugonga vichwa vya habari vilivyo Bongo baada ya kuweka wazi kuwa yupo mbioni kuolewa.

Sasa Esha Buheti amemueleza Wema kuwa anawaumiza mashabiki wake kwa kuweka mambo yake binafsi kwenye mitandao.

Hata hivyo muingizaji Jackline Wolper amemvaa Esha Buheti na kumueleza kuwa angemshauri Wema kistaaribu na sio kuweka wazi. Kupitia ukarasa wake Instagram Wolper ameandika;

"Baby Esha anayeumia na Wema anaumia Inbox na watu wake na anakosa mpaka hadi nguvu ya kuandika Insta lakini hadi nguvu ya kuandika Insta mmh yaangalie vizuri maumivu yako yanachembechembe za virusi vya unafiki," ameeleza Wolper.

Naye Esha Buheti alijibu hilo kwa kueleza kuwa; "Yeye anayaposti inbox?, nakuheshimu sana sijawahi kukuvunjia heshima so please na umeona kuna lolote baya nimeongea?, nakuomba sana sana Jackie niachee nakuheshimu sana,".