Jinsi ya kuruka vihunzi vya mwanume anayekutongoza mara kwa mara


Miongoni mwa kero ambazo huwakumbuka wadada wengi ni pamoja na kutongozwa, jambo hili  huwa halikwepeki kwani lipo tu. Hivyo kama wewe ni msichana ambaye upo  kwenye mahusiano na bado unaendelea kukutana na ushawishi wa kutongozwa kila iitwapo leo pindi ukutapokutana na mtu ambaye anakutongoza unatakiwa kuwa hivi.

1. Usijibu mtu huyo simu wala texts zake. 

Kitu cha kwanza cha kufanya ni kuhakikisha kuwa haujibu simu zake wala kumtext hata kama umeboeka. Ukiwa unajibu simu zake basi utakuwa unampa matumaini kuwa uko interested na yeye. Ukimzima baada ya muda flani bila shaka atakuja kuelewa – ama unaweza tu kumpa ile hotuba ya kuwa wewe na yeye hamulingani.

2. Mblock katika mitandao ya kijamii. 

Kando na kuwa hujibu sms zake wala simu zake, unapaswa kublock contacts zake zote katika mitandao ya kijamii ambazo unazijua. Kama unahisi kumblock utakuwa umevuka mipaka yakuonekana mbaya, na unaona si tishio kwako, basi angalau fanya kumdelete.

Kumuweka katika contacts zako kutampa hisia ya kuwa nyinyi wawili mna connection aina flani, aidha ya kibinafsi au kikazi, hivyo kuona kuwa ni haki yake kuwasiliana na wewe.

3. Badilisha namba yako ya simu. 

Najua utahisi vibaya kubadilisha namba yako ya simu, lakini kama mwanaume atakuwa anaendelea kukupigia simu na kukutext mara kadhaa kwa siku, ilhali tayari amejua kuwa huko interested na yeye, basi itakuwa jambo la kufanya ili kujiokoa.

Pindi utakapojeuza namba yako, usijaribu kuiweka sehemu yeyote online, kwa sababu huyu mwanaume ama rafiki yake anaweza kuiona. Pia hakikisha kuwa marafiki zako hawapeani namba yako ya simu kwa yeyote.

4. Jifanyishe kuwa una boyfriend/mume

 Wakati mwingine huyu nuksi akifikiria kuwa una boyfriend au mume, atatulia na kuachana na wewe kabisa na kufuata mwanamke mwingine. Hii ni kweli haswa iwapo huyu nuksi ni mwanaume mwoga ama mwenye haya.

Ukianza kumwambia huyu mwanaume nuksi kuwa wewe hauko single, basi mwisho ataenda zake. Kama hatareact na hizi habari mpya, unaweza kutafuta mwanaume mwenye miraba halafu umfanye kuwa ni boyfriend wako wakati unamwona yuko karibu.