'Kesi ya T.I yaanza kuwa nyepesi'

Rapper kutokea nchini Marekani, T.I amefutiwa shtaka lilokuwa likimkabili la kuwashambulia walinzi kwenye geti la makazi ya jumuiya ambapo pia anaishi mjini Atlanta.

Inaelezwa kuwa T.I aliwashambulisha walinzi hao Mei 28, 2018  a Shtaka hilo lililfunguliwa July mwaka huu ikiwa ni miezi miwili baada ya kutokea.

Licha ya shtaka hilo kufutwa, T.I. bado anakabiliwa na makosa mawili: Kulewa hadharani pamoja na mwenendo mbaya wa tabia.  Rapper huyo alikuwa akishtakiwa kwa kosa la kuwashambulia walinzi hao huku akiwa amelewa kupitiliza.