Kocha wa Simba afumua kikosi kuja na mfumo mpya


Kocha Mkuu wa timu ya Simba raia wa Ubelgiji Patrick Aussems, amefumua kikosi cha Simba na kuamua kuja na mfumo mpya ili aweze kushinda  leo dhidi ya Stand United utakaochezwa uwanja wa Taifa.

Mbelgiji amefikia hatua hiyo kutokana na safu ya ushambuliaji kushindwa kuwa makini  kutumia nafasi wanazozipata.

"Washambuliaji wangu wote wanakosa umakini wanapokuwa katika lango nimeliona na nimelifanyia kazi,nimewapa mbinu mpya ambazo zitasaidia kupata ushindi mapema.

"Kwa sasa kila mchezaji nimemfundisha kufunga kwa mbinu zote ili kuwarahisishia washambuliaji kazi hasa wanapopata nafasi nao wataweza kufunga,natarajia mabadiliko makubwa ndani ya kikosi"alisema.