Masoud Djuma afunguka kuhusu Mo


Aliyekuwa kocha Msaidizi wa timu ya Simba Masoud Djuma, sasa ni kocha Mkuu wa timu ya As Kigali inayoshiriki ligi kuu nchini Rwanda ametoa ya moyoni kuhusu kupatikana kwa Mo.

Djuma amesema ni jambo la kumshukuru Mungu hasa kwa muwekezaji na mfanyabiashara Mohamed Dewji "Mo" kurejeshwa salama.

"Mungu ametenda miujiza yake ,kitu kikubwa ambacho kinazidi kuongeza furaha kwa watanzania pamoja na mashabiki wa Simba,naamini kilichosaidia kumrejesha ni dua za watanzania na
dunia"alisema.