10/11/2018

Mbaroni kwa kumbaka na kumnyonga mtoto wa miaka nane


Jeshi la polisi mkoani Mbeya linamshikilia mkazi wa kata ya Upendo wilayani Chunya Masanja Willy (25) kwa tuhuma za kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka minane, Kwangu Bundala ambaye alikuwa mwanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya msingi Upendo kisha kumnyonga na kumuua.

Afisa Mtendaji wa kata ya Upendo, Lucas Alan Mwangala ambaye ndiye aliyetoa taarifa polisi kuhusiana na tukio hilo la ubakaji amesema wananchi baada ya kupata taarifa za kubakwa kwa mtoto huyo walishirikiana na polisi kumkamata mtuhumiwa na kumfikisha kituo cha polisi ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.