https://monetag.com/?ref_id=TTIb Mwenyekiti wa halmashauri ya Kilwa awapongeza waliomkamata | Muungwana BLOG

Mwenyekiti wa halmashauri ya Kilwa awapongeza waliomkamata

Na.Ahmad Mmow, Kilwa.

IKIWA ni siku chache tu tangu akamatwe kwa tuhuma za kukutwa na mbao zilizovunwa kinyume cha sheria.Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kilwa,Abou Mussa Mjaka amewakingia kifua nakuwapongeza waliomkamata na kumfikisha kituo cha polisi.

Mjaka amebainisha hilo,leo katika mamlaka ya mji mdogo wa Kilwa Masoko alipozungumza na Muungwana kuhusu tukio la kumakatwa kwake kuhusiana na tuhuma za kukutwa na mbao zilizovunwa kinyume cha sheria.Tuhuma ambazo katika mazungumzo hayo alikiri kuwa nizakweli.

Mjaka alisema waliomkamata hawapaswi kulaumiwa,bali wanasitahili kupongezwa kwakusimamia na kulinda maliasili na rasilimali za wilaya hiyo na taifa.Kwani nimiongoni mwa mambo ambayo yeye,madiwani wenzake na chama chake(CUF) wanahimiza na kupigia kelele yafanyike.

"Mimi nawenzangu katika chama na baraza la madiwani tunahimiza ulinzi na usimamizi mzuri wa rasilimali na maliasili zilizopo katika halmashauri yetu na taifa.Kwahiyo wale niwakuwapongeza badala ya kuwakatisha tamaa,"alisema kwa kwa ujasiri Mjaka.

Mbali na kuwapongeza maofisa wa  wakala wa huduma za misitu(TFS) na jeshi la polisi ambao walikwenda kumkamata mwenyekiti huyo, alitoa wito kwa watu wanaohusisha kukamatwa kwake na itikadi za siasa waachane na dhana hiyo.

Alisema kukamatwa kwake hakuhusiani na itikadi za siasa na haamini kama kulitokana na shinikizo kutoka kwa wanasiasa.Bali kilichofanyika nikitu cha kawaida ambacho kipo kwa mujibu wa sheria.Kwasababu serikali isingeacha kutimiza wajibu wake kwakuwa  yeye nimwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo na anatokea chama cha upinzani.Kwani sheria zipo kwaajili ya watu wote.

Alipoulizwa kwanini alikuwa na mbao zilizovunwa kinyume cha sheria.Alisema alinunua kwa mfanyabiashara halali wa mbao.Ambae hata TFS inamtambua.Kwasababu ametimiza na kutekeleza masharti yote yanayomuwezesha kufanya biashara hiyo.

Aliweka wazi kwamba kilichomponza nikununua mbao zisizigongwa.Jambo ambalo nikosa.Hata hivyo muuzaji alimuhakikishia zilikuwa zimegongwa.Nae alikuwa hajui nampaka sasa hajui  tofauti ya mbao zilizogongwa na zisizogongwa.Kwasababu hana ujuzi huo.

"Kuhusu hilo nitoe wito kwa wataalamu na watumishi wa sekta ya misitu watoe elimu yakutosha kuhusu jinsi ya kutambua mbao zilizogongwa kihalali,ziligongwa kinyume cha sheria na zisizogongwa kabisa.Nilinunua kwanjia halali na sehemu halali lakini bila kujua nilinunua bidhaa isiyohalali. ," alisema kwa masititiko Mjaka.

Aidha alikiri kwamba mbao hizo zipo mikononi mwa serikali.Nakwamba haziwezi kuwa mali yake tena.Kwani  sheria itachukua mkondo wake.Ikiwemo kutaifisha,kupigwa mnada na taratibu nyingine kwa mujibu wa sheria za nchi.

Hivi karibuni mwenyekiti huyo diwani wa kata ya Masoko(CUF) alikamatwa na kusababisha alale rumande kwatuhuma za kukutwa na vipande vya mbao takribani 400 ambazo hazikuwa na nyaraka zilizothibitisha uhalali wake.