https://monetag.com/?ref_id=TTIb Njia Rahisi Za Kujitibu Ugonjwa Wa Fangasi za mdomoni | Muungwana BLOG

Njia Rahisi Za Kujitibu Ugonjwa Wa Fangasi za mdomoni


Benson Chonya
Asilimia 35-50% ya watu duniani wana fangasi mdomoni. Kuna aina nyingi wa fangasi lakini wale wanaoitwa candida albicans ni wengi zaidi.

Fangasi hawa huishi bila kusababisha madhara yoyote pale ambapo mazingira ya mdomoni hayatabadilika.

Hata watoto wadogo wanapozaliwa hupatwa fangasi hawa kutoka kwenye uke wa mama zao, ndio maana mama anashauriwa kumnyonyesha mtoto Mara tu baada ya kujifungua ili ampatie kinga dhidi ya magonjwa ikiwemo ya fangasi.

Fangasi hawa huwa wengi sana kiasi cha kuleta madhara kwa watu wanaokula vyakula vya sukari kwa sana, wanaotumia madawa sana kama tetracycline na corticosteroids ambazo hushusha kinga ya mwili. Pia kwa wavutaji wa sigara na waathirika wa UKIMWI, kisukari, saratani na wale wanaovaa meno bandia.

Mara nyingi ugonjwa wa fangasi mdomoni (oral candidiasis/ oral thrush) inatokana na kubadilika kwa mazingira mdomoni kuliko kusema inasababishwa na wadudu.

Dalili za ugonjwa huu.
Vidonda au tishu za mdomoni kuharibika bila maumivu au wakati. mwingine maumivu kama kuwaka moto.


  • Ladha ya chuma, tindikali, chumvi au uchungu mdomoni.
  • Ugumu katika kumeza.
  • kukwaruza kwa sauti.

Si dalili zote zitaonekana kwa watu wote. Moja au zaidi zinaweza kujitokeza kwako.

Jinsi ya kujitibu.
1. Maziwa mgando
Maziwa mgando yakitumiwa na mtu mwenye fangasi mdomoni kama kinywaji kila siku asubuhi na jioni, kuanzia wiki moja na kuendelea inaweza kusaidia kurudisha hali ya kawaida ya mdomoni na kupona kabisa.

2. Usafi wa kinywa.
Kinywa kisafishwe kila baada ya mlo na sio kila unapoamka kama ilivyo mazoea ya watu wengi. Pia dawa inayotumiwa ni vema ikawa ni ile yenye kemikali ya kuua vimelea vya magonjwa. Pia kama unatumia meno sanifu hakikisha unayafanyia usafi vema kama ulivyoelekezwa.

3. Antibiotics
Kama kwa kutumia matibabu hapo juu hayajasaidia unaweza kutumia dawa zifuatazo kwa maelekezo ya daktari, nystalin, miconazole, gentian violet au amphotericin B.