Real Madrid hoi yatandikwa nyumbani na Levante


Ligi kuu nchini Hispania La Liga imeendelea leo ambapo timu ya Real Madrid imekubali kichapo kwenye uwanja wa nyumbani, Santiago Bernabeu mabao 2-1 na Levante

Katika mchezo huo wa La Liga timu ya Levante ilifanikiwa kupata bao dakika ya sita likifungwa na Jose Luis Morales huku Roger Marti akipachika bao la pili dakika ya 13 kwa penalti kabla ya Marcelo kuifungia Real Madrid la kufutia machozi dakika ya 72