https://monetag.com/?ref_id=TTIb Viongozi wa Serikali watakiwa kutumia ilani ya CCM | Muungwana BLOG

Viongozi wa Serikali watakiwa kutumia ilani ya CCM


Na. Thabit Madai, Zanzibar
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Ayoub Mohammed Mahmoud Amewataka viongozi wa Shehia ndani ya Mkoa huo kutekeleza majukumu yao kwa kufuata ilani ya chama cha Mapinduzi CCM.

Alisema hatua hiyo itawasaidia watendaji hao wa shehia kufanya kazi sambamba na sera ya serikali ya mapinduzi ya Zanzibar.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa kumuapisha sheha wa shehia ya Jang’ombe urusi Yussuf Juma mtumwa pamoja na  kumteua kaimu sheha wa shehia ya chuini Mohameed Kheri mara baada ya kutenguliwa kwa sheha wa shehia hiyo hivi karibuni,

RC Ayoub amesema ilani ya chama cha mapinduzi ndiyo inayoongoza nchi hivyo watendaji wa serikali kuanzia serikali za mitaa hadi serikali kuu wanapaswa kusoma, kuelewa pamoja na kuitekeleza kwa vitendo ilani ya chama cha Mapinduzi CCM.

" Hatua hiyo itasaidia kujenga maelewano na uaminifu baina yao na wananchi pia itasaidia wananchi kuweza kupeleka kero zao na kupatiwa ufumbuzi kwa urahisi” alisema Ayoub.

Kwa upande mwingine aliwataka viongozi hao wapya kuweza kushoirikiana na wananchi katika kuyatafutia ufumbuzi matatizo wanayokabiliana nayo katika shehia zao.