Vyakula Vinavyoongeza Nguvu na Akili katika Ubongo wa Mwanadamu



Kuna wakati unaona wazi ubongo wako umechoka au ufanisi wake umepungua tofauti na zamani. Au sababu tu ya kazi na misongamano mingi unajikuta kichwa kimechoka kufanya kazi.

Hakuna dawa yoyote hospitalini inayoweza kukurudishia nguvu zako za ubongo. Dawa nyingi za kizungu za kuongeza nguvu za ubongo zina madhara makubwa baadaye katika mwili.

Kila mmoja wetu anapatwa na tatizo hili la kuhisi kushuka kwa nguvu za ubongo wake. Takwimu zinaonyesha baada ya miaka 85 uwezekano wako wa kupata ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu huongezeka kwa asilimia 50.

Hivyo ni wazi tunahitaji kujiwekea mazoea na tabia ya kula vyakula na kuishi namna ambazo zitakuwa zikiendelea kuupa nguvu ubongo kila siku.

Hapa nimekuandalia orodha ya haraka haraka ya vyakula hivyo, pia uhakikishe unapata usingizi wa kutosha kila siku:


  • Mafuta ya zeituni
  • Mafuta ya nazi.
  • Samaki.
  • Binzari
  • Mayai
  • Korosho
  • Mazoezi ya viungo
  • Broccoli
  • Parachichi
  • Mvinyo mwekundu
  • SpinachiLozi (Almonds)
  • Mbegu za mabogaKitunguu swaumu