https://monetag.com/?ref_id=TTIb Vyakula vinavyoongoza kupunguza mafuta tumboni kwa wanawake | Muungwana BLOG

Vyakula vinavyoongoza kupunguza mafuta tumboni kwa wanawake


Benson Chonya
Wanawake wengi miaka ya karibuni wanakabiliwa na tatizo linalofanana na kitambi kwa upande wa wanaume. Hivyo ingekuwa ni wanaume tungesema ni kitambi ambalo nalo ni tatizo kubwa miongoni mwa wanaume wengi nyakati za sasa.

Kinachowasumbua wanawake siyo kitambi tunasema ni mrundikano wa mafuta sehemu ya chini ya tumbo na tumbo kwa ujumla kufikia hali kuonekana kama ana tumbo kubwa au kuhisi labda ni ujauzito kumbe ni mafuta mengi.

Hali hii imeshamiri hasa kwa mama waliojifungua  na kupoteza muonekano wao wa kirembo lakini kikubwa zaidi wapo katika hatari ya kupata magonjwa kama kisukari, matatizo ya moyo, kiharusi (stroke), shinikizo la juu la damu  nk.

Vyakula  vinavyoondoa mafuta kwenye tumbo kwa wanawake

1. ASALI NA LIMAU
Chukua asali kijiko kikubwa kimoja cha chakula na majimaji ya limau vijiko vikubwa viwili, changanya hivi viwili ndani ya glasi moja (robo lita) ya maji ya uvuguvugu na unywe yote mara tu ukiamka asubuhi.

Tumia kwa wiki 3 hivi mpaka mwezi mmoja na hutachelewa kuona tofauti.

2. MAJI YA UVUGUVUGU
Kunywa maji ya uvuguvugu kama lita 1 hivi wakati tumbo likiwa tupu hasa asubuhi ukiamka tu. Hii inasaidia kusafisha mwili na kuondoa mafuta yasiyohitajika.

3. NYANYA
Kula nyanya ambazo hazijapikwa pia inasaidia kupunguza tumbo kwa kina mama, hivyo kula kachumbali ya kutosha kila siku ya nyanya peke yake na utaona mabadiliko.

4. TANGAWIZI
Chemsha chai ya tangawizi, ipua na usubiri ipoe kidogo, ongeza asali mbichi kidogo na pilipili manga kidogo ya unga. Pata kikombe kimoja cha chai hii kila siku asubuhi mapema ukiamka tu. Asali inasaidia kuyeyusha mafuta wakati pilipili itauongezea nguvu mfumo wa mmeng'enyo wa chakula.

5. SIKI YA TUFAA
Siki ya tufaa (apple cider vinegar) inasaidia kupunguza njaa na kukufanya ujisikie umeshiba kwa kipindi kirefu. Kunywa kijiko kikubwa kimoja cha siki ya tufaa mara 1 kwa siku kila siku wakati unakula chakula cha usiku. Kazi nyingine ya hii siki ni kuweka sawa damu sukari mwilini hivyo ni nzuri pia kwa wenye kisukari.

6. MAJANI YA BIZARI
Majani ya bizari husaidia kuondoa sumu na takatka nyingine mwilini kitu ambacho moja kwa moja hupelekea mlundikano mdogo wa mafuta katika tumbo. Kunywa chai ya majani ya bizari kila siku asubuhi, ukikosa majani unaweza kutumia hata unga wake.

8. ILIKI
Iliki hufanya kazi ya kuongeza nguvu katika mfumo wa mmeng'enyo wa chakula na ni dawa nzuri sana ya kuondoa sumu na takataka nyingine mwilini. Iliki pia hutumika katika kupunguza uzito. Tengeneza chai yenye iliki kila siku ndani yake, pia ni kiungo karibu kwa vyakula vingi hivyo hakikisha unaiweka katika kila chakula unachopika kwa matokeo mazuri zaidi.

9. MDALASINI
Mdalasini hufanya kazi ya kuchoma mafuta mwilini. Chukua kijiko kidogo kimoja cha mdalasini ya unga na uweke ndani ya glasi 1 ya maji ya moto na uache kwa dakika 5 hivi. Ongeza kijiko kidogo kimoja cha asali mbichi ndani yake na ukoroge vizuri, kisha unywe huo mchanganyiko wote asubuhi ukiamka tu.

10. JUISI YA LIMAU
Kunywa maji ya limau au juisi ya limau kila mara kutakusaidia kuondoa mafuta tumboni kwa haraka sana. Ongeza majimaji ya limau vijiko vikubwa viwili ndani ya glasi 1 ya maji na uongeze punje 1 ya chumvi ya mawe, koroga vizuri na unywe asubuhi ukiamka tu kila siku.

11. KITUNGUU SWAUMU
Ili kupunguza mafuta tumboni katakata vipande vidogo vidogo (chop) punje 3 mpaka 4 za kitunguu swaumu na unywe na maji vikombe viwili asubuhi tu na kisha shushia na glasi moja ya maji yenye limau kidogo kwa mbali. Hii ndiyo njia nzuri kabisa ya asili ya kuondoa mafuta tumboni kwa haraka zaidi.

12. TIKITI MAJI
Tikiti maji lina asilimia 82 za maji kitu kinachofanya tumbo lako kutokuwa na njaa ya kuhitaji chakula. Tikiti maji lina vitamini C ambayo ni mhimu kwa afya bora. Kula tikiti kila siku.

13. MAHARAGE
Kula maharage kila mara kunasaidia kupunguza mafuta katika tumbo. Maharage yana kiasi kingi cha nyuzinyuzi (faiba) kitu kinachosaidia tumbo lako kutojisikia njaa na hivyo itakuwezesha kula chakula kiasi kidogo. Kadri unavyokula chakula kichache ndivyo unavyokuwa mbali na uwezekano wa kuzalisha mafuta mengi tumboni.

14. TANGO
Tango lina asilimia 96 za maji na asilimia zinazobaki ni nishati. Tumia kachumbali yenye tango ndani yake kila siku au kula tu tango moja kila siku ili kupunguza mafuta tumboni kwa haraka.