Wanajeshi kuchuana Leo Uwanja wa maji maji Ligi daraja la pili


Na John Walter-Manyara

Baada ya kuwasili salama mkoani Ruvuma, kikosi cha  Usalama Sc ya daraja la pili, leo jioni kinashuka dimbani kucheza mchezo wao wa kwanza wa ligi daraja la pili dhidi ya Wanajeshi The Might Elephant.

Mchezo huo utakuwa wa aina yake kwani timu zote zinatokana na Vikosi vyetu vya Ulinzi wa Amani hapa nchini, Usalama Sc kutoka Mkoani Manyara inatoka Jeshi la Polisi huku The Might Elephant ya Ruvuma ikitoka Jeshi la wananchi wa Tanzania [JWTZ]   

Taarifa zinaeleza Usalama Sc watashusha kikosi chao kamili katika mchezo huo dhidi ya The Might Elephant FC  ambao utakaoanza majira ya saa 10 kamili jioni.


Msemaji wa timu ya Usalama Sc Ramadhani Masudi Fupe katika Mitandao ya kijamii amewaomba wana Manyara kuiombea dua timu yao ili iweze kufanya vizuri.

Aidha kwenye Group lao la Whatsap mmoja kati ya viongozi wa timu Mkumbo John,amepost picha vijana wakiwa mazoezini  na kuandika haya “Tukiwa mazoezini leo asubuhi kwenye uwanja wa Maji maji,vijana wote tupo timamu hakuna majeruhui hata mmoja na wanaonekana wenye hari kubwa ya kupata ushindi,tutegemee ushindi tu na sio sare wala kushindwa.”

Furaha ya Viongozi wa Timu  ya Usalama Sc wakiongozwa na walezi wa timu Kamishna Msaidizi wa jeshi la Polisi SACP Agustino Senga na Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya jinai wa Mkoa wa Manyara (RCO) Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Joshua Mwafulambo ,ni pale timu hiyo itakapoibuka na ushindi katika mchezo wao wa kwanza katika msimu huu wa ligi daraja la pili dhidi ya wanajeshi hao waliopigana vita vya Maji maji Songea .