https://monetag.com/?ref_id=TTIb Wananchi wa Kijiji cha Ngereani wamuangukia Waziri wa Maji | Muungwana BLOG

Wananchi wa Kijiji cha Ngereani wamuangukia Waziri wa Maji


Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Wananchi wa Kijiji cha Ngereani kitongoji cha Lokii kilichoko Wilayani Longido wamelalamikia kero ya maji inayowasababisha wamama kutafuta maji umbali mrefu hata nyakati za usiku hivyo wamemuomba Naibu Waziri wa maji Juma Aweso awapatie kituo cha maji kutoka katika mradi wa maji yanayotoka Mto Simba ulioko Wilaya ya Haimkoani Kilimanjaro  kwenda Wilaya ya Longido .

Wakizungumza na Kiongozi huyo wamesema kuwa kijiji hicho hakina huduma za maji salama kwa matumizi ya binadamu pamoja na kunywesha mifugo yao.

Wanakijiji hao Kijiji Lilian Mbokwa na  Luka Lakaneti wamesema kuwa iwapo watapatiwa tawi la mradi wa maji unaopita kijijini hapo itawasaidia wananchi hao kupata huduma hiyo muhimu.


Naibu Waziri wa Maji Juma Aweso ameitaka Mamlaka ya Maji safi ya Arusha (AUWSA) kuhakikisha kuwa wanawaunganishia wananchi hao Maji ili kuondokana na kero ya Maji kwani serikali imelenga kutatua changamoto hizo .

Mwenyekiti wa Bodi ya Maji Dk.Richard Masika wamesema kuwa mamlaka hiyo inalenga kutatua kero ya uhaba wa Maji kipitia mradi Mkubwa unaondelea wa upanuzi wa vyanzo vya Maji.

Mkurugenzi wa (AUWSA) Injinia Ruth Koya wamesema kuwa kwasasa wako katika hatua nzuri ya utekelezaji na inatarajia kukamilika mwaka 2020.