https://monetag.com/?ref_id=TTIb DC Katambi: Nitawashughulikia watendaji wanaoleta migogoro ya ardhi | Muungwana BLOG

DC Katambi: Nitawashughulikia watendaji wanaoleta migogoro ya ardhi



Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi amesema atawashughulikia watendaji wote ambao wamekuwa wakichangia uwepo wa migogoro ya ardhi.

DC Katambi ameyasema hayo wakati alipokua akijibu swali la wandishi wa habari waliotaka kujua hatua gani ambazo atachukua ili kuweza kuzuia migogoro ya ardhi ambayo imekua ikilalamikiwa na wananchi wa wilaya hiyo.

Amesema ni kweli kuna migogoro ya ardhi lakini kwa taaluma yake kama mwanasheria bado hakuna mgogoro ambao umeshindwa kutatulika.

“Utaratibu wa kuitatua migogoro inafahamika, suala ni nia njema ya kutatua migogoro hiyo lakini mimi huwa nasema kama migogoro inaendelea kuwepo basi ni mambo mawili, mosi ni hatuna uwezo wwa kuitatua au pili tuna maslahi kwenye ardhi, kama hatuna maslahi na tuna uwezo basi uwezo wa kuitatua tunao.

“Nafahamu kuna watendaji ambao wakati mwingine wanajiingiza kutengeneza migogoro na watu sisi tumesema awamu ya tano hatutaki mchezo kwenye hili na mimi nitawashughulikia hata awe nani ilimradi nina nguvu kama Mkuu wa Wilaya sitomuacha mtu alete mgogoro,” amesema Katambi.

Aidha amesema atakaa kikao na watu wote wenye hati kwa mujibu wa sheria ili kukubaliana na siyo kuoneana kwa kufanya vikao bila kuwashirikisha wamiliki wa ardhi.