India yakumbwa na kimbunga kikali

Kimbunga kikali kilicho athiri maeneo ya mashariki mwa India watu 10 wamepoteza maisha.

Kiongozi wa kitaifa wa usimamizi wa maafa nchini humo Narendra Kumar amesema maeneo ya pwani ya  jimbo la Tamil Nadu kimbunga Gaja kimesababisha vifo 10 na kuharibu idadi kubwa ya nyumba.

Kumar amesema watu zaidi ya elfu 80 wamehamishwa kutokana na kimbunga hicho. kimbunga hicho ambacho upepo wake  ulikuwa mwendo kasi wa kilomita 90 kwa saa kimesababisha kukuosekana kwa umeme vile vile mashule yamefungwa kwa muda katika maeneo yaliyoathirika.

Mwaka 1999 katika jimbo la Orissa nchini India zaidi ya watu elfu 15 walipoteza maisha kutokana na kimbunga kilichotokea mwaka huo.