https://monetag.com/?ref_id=TTIb Kocha Simba azitaka mechi hizi mbili kujipima nguvu | Muungwana BLOG

Kocha Simba azitaka mechi hizi mbili kujipima nguvu


Wakati kikosi cha Simba kikiwa katika mapumziko, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mbelgiji, Patrick Aussems amesema anahitaji mechi kadhaa za kirafiki kwa ajili ya kuiweka fiti zaidi timu.

Aussems ameeleza kuwa anahitaji mechi mbili ili kuwafua vilivyo wachezaji wake kwakuwa hivi sasa hawana mechi yoyote ile mpaka Taifa Stars imalizane na Lesotho.

Mbelgiji huyo ameamua kuwaweka wachezaji wake katika morali ambapo anataka kuhakikisha hawachuji bali waendeleze moto uleule.

Kocha huyo amehitaji mechi moja inayohusisha timu ya hapa Tanzania na nyingine iwe ya nje ya nchi ili kuwapa moto zaidi vijana wake.

Simba wamezidi kujifua jijini Dar es Salaam huku nyota wake wengi takribani 12 wakiwa na vikosi vyao vya timu za taifa kuzitumia kwa ajili ya kuwania kufuzu kuelekea AFCON 2019.