Kocha wa Simba akataa kusajili mchezaji kutoka Yanga

Kocha mkuu wa klabu ya Simba apingana na uongozi wa timu hiyo kuhusu uwezo wa kiungo mshambuliaji wa Yanga.

Hayo yamekuja baada ya viongo wa Simba kuvutiwa na uwezo wa mchezaji huyo kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara

Patrick Aussems amesema kuwa kwa sasa hajavutiwa na mchezaji yoyote kutoka ndani ya Yanga hivyo Ajibu inabidi asubiri wakati mwingine kurudi Msimbazi.

"Hakuna mchezaji ambaye amenivutia kutoka ndani ya Yanga hivyo sina chaguo lolote la kumsajili mchezaji wa Yanga katika dirisha dogo kuimarisha kikosi," alisema.

Ajibu amekuwa na mwanzo mzuri kwenye ligi kwa kuwa amekuwa msaada ndani ya timu yake kwa kuhusika kutengeneza pasi 9 za mabao na kufunga mabao 3 kati ya 17 waliyofunga Yanga.