https://monetag.com/?ref_id=TTIb Lady Jaydee aeleza sababu za kumfollow Khadija Kopa mtandaoni | Muungwana BLOG

Lady Jaydee aeleza sababu za kumfollow Khadija Kopa mtandaoni


Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Lady JayDee ameeleza sababu za kumfollow, msanii wa nyimbo za Taarabu, Khadija Kopa kwenye mtandao wake wa Instagram.

Lady Jaydee amesema kuwa Khadija ni msanii anayempenda siku zote na anatamani kujua anafanya nini huku akieleza kuwa kwa upanda mwingine ni Role mode wake.

"Marafiki zangu wengi huwa naona sababu ya kuwafollow sina kwasababu nakuwa nao mara nyingi najua kila kitu wanacho kifanya na tuna chat watsapp kila saa Khadija Kopa mimi ni role mode wangu yaani mtu ambaye nampenda siku zote huwa napenda kujua anafanya nini," amesema Jide.