https://monetag.com/?ref_id=TTIb Mambo 14 yaliyotolewa na Waziri Mkuu wakati akitoa hoja ya kuhairisha Bunge | Muungwana BLOG

Mambo 14 yaliyotolewa na Waziri Mkuu wakati akitoa hoja ya kuhairisha Bunge



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo amezungumza mambo mbalimbali wakati akitoa hoja ya kuhairisha Bunge. Haya ni baadhi ya mambo aliyoyazungumza Waziri Mkuu akiwa Bungeni.

1. Natoa rai kwa Wabunge waliochaguliwa kuwatumikia wananchi kama walivyoahidi.

2. Serikali iliunda Tume ya kuchunguza chanzo cha ajali ya Kivuko cha MV Nyerere, tayari tumepokea taarifa hiyo na tunaendelea kuifanyia kazi .

3. Matukio ya ajali za bararani yamepungua kutoka ajali 9856 mwaka 2016, ajali 5578 mwaka 2017 na kufikia ajali 3209 katika kipindi cha Januari hadi Oktoba 2018.

4. Katika kipindi cha mwezi Julai hadi Oktoba 2018, Serikali imepeleka moja kwa moja kiasi cha shilingi Bilioni 38.6 katika shule za Msingi na shilingi bilioni 44.6 zilipelekwa shule za Sekondari.

5. Tangu kuanzishwa kwa elimu bure,uandikishwaji wa watoto wa awali na darasa la kwanza umeongezeka pia ufaulu wa mitihani ya darasa la saba umeongezeka kutoka wastani wa asilimia 70 mwaka 2016 hadi wastani wa 78 mwaka 2018.

6. Kupitia Program ya Lipa Kulingana na Matokeo katika Elimu, jumla ya shilingi Bilioni 53.4 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya shule za Msingi na Sekondari.

7. Shilingi Bilioni 9.2 zimeelekezwa katika kuimarisha miundombinu ya elimu kupitia Program ya Kuboresha Elimu ya Shule za Msingi.

8. Nawapongeza wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto na Bumbuli kwa uhifadhi mzuri wa mazingira, naziagiza halmashauri zingine kuiga mfano huo.

9. Namshkuru Rais Magufuli kwa maelekezo yake mahsusi kuhusu namna bora ya uendeshaji wa biashara za mazao, natoa rai kwa sekta binafsi kulinda maslahi ya wakulima na Taifa kwa ujumla.

10. Kupitia maonesho ya viwanda na teknolojia ya madini, wajasiriamali wa sekta ya madini walipata fursa ya kukutana na wataalam na kujifunza teknolojia bora ya uchenjuaji madini ambayo ni rafiki wa mazingira  pamoja na kufahamu taratibu mbalimbali za kupata mikopo.

11. Serikali inawahakikishia wananchi kuongeza kasi katika kutekeleza na kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kadri hali ya uchumi itakavyokuwa inaruhusu.

12. Serikali iliamua kutunga sheria ndogo za fedha ya mwaka 2018 kwa lengo la kuongeza udhibiti wa sekta hiyo pamoja na kuiwezesha kuchangia ipasavyo katika kuimarisha uchumi wa nchi na kulinda mali na fedha za wananchi wetu.

13. Nawatakiwa heri na maandalizi mema ya ushindi kwa timu ya Taifa ya mpira wa miguu (TAIFA STARS) dhidi ya timu ya Taifa ya Lesotho.

14. Naahirisha vikao vya bunge hadi Januari 29, 2019 saa 3: 00 asubuhi.