Marekani yamjumuisha kwenye orodha ya vikwazo raia wa Afrika kusini

Marekani yamuingiza katika orodha ya vikwazo raia wa Afrika kusini mwenye asili ya Urusi kwa madai kwamba raia huyo ameisaidia Korea ya Kaskazini kufanya biashara.

Waziri wa Hazina wa Marekani alisema raia huyo wa Afrika kusini aliyezaliwa Urusi, Vladlen Amtchentsev, alifanya shughuli ambazo sio halali kwa niaba ya serikali ya Pyongyang. Na anaadhibiwa kwa makosa hayo ya kuiwakilisha serikali ya Pyongyang.

Taarifa ilyotolea na Hazina ya Marekani inasema Amtchentsev alitoa ushauri kwa Korea Kaskazini na kuliwezesha taifa hilo kuvikwepa vikwazo vilivyowekwa na Marekani ni hivyo kufanikiwa kununua mafuta. Marekani pia imeliweka katika orodha hiyo ya vikwazo shirika la Velmur Management kwa kuhusiana na kadhia hio.