Mchezo wa Simba na Lipuli FC wasogezwa mbele

Mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kati Simba na Lipuli FC ambao ulikuwa umepangwa kuchezwa kesho Jumatano 21/11/2018 umesogezwa mbele na sasa utachezwa siku ya Ijumaa 23/11/2018.

Mabadiliko hayo yamefanywa ili kuwapa nafasi wachezaji waliokuwa kwenye timu zao za Taifa kujiunga na vikosi vyao ili kuwa sehemu ya wachezaji ambao watacheza mchezo huo.

Wakati huo huo, Simba itamkosa beki wake wa kulia Shomari kapombe ambaye ameumia akiwa kambini na timu ya taifa 'Taifa Stars'.

Tayari Kapombe ameshaanza kufanyiwa matibabu huko Afrika Kusini ili kurejea katika hali yake ya kawaida hapo baadaye.