https://monetag.com/?ref_id=TTIb Msami: Nina bahati ya kuwa na watoto wazuri | Muungwana BLOG

Msami: Nina bahati ya kuwa na watoto wazuri


Msanii wa Bongo Flava na Dancer, Msami  amesema kuwa ana bahati ya kuwa kwenye mahusiano na watoto wazuri kwasababu anapotoka mtoto mzuri anaingia mwingine lakini sio lazima awe anatoa taarifa.

Msami amesema kuwa wanachotakiwa wao kama wasanii nikuleta muziki mzuri ishu za mapenzi ni maisha ambayo yapo kila siku.

"Mimi nina bahati ya kuwa na watoto wazuri anapotoka mtoto mzuri anaingia mtoto mzuri lakini sio lazima tuwe tunatoa taarifa tunachotakiwa kukileta hapa ni muziki kama natoa muziki mzuri watu wanaupenda hayo maisha mengine ya mapenzi ni maisha tu ambayo yapo kila siku mi ya zamani sikuyaleta nyie ndio mlikuwa mnayataka," amesema Msami.

Kauli hiyo imekuja baada ya kuhojiwa kuwa tangu aachane na msanii wa filamu, Irene Uwoya imekuwa kama amepotea kwenye game.