Kwa mra ya kwanza nchini Marekani, wanawake wawili wakiwa wenye imani ya uislamu kutoka Somalia na Palestina wameshinda katika uchaguzi na kuingia katika bunge la Marekani.
Rashida Tlaib ana asili ya Palestina, baba yake alikimbia Palestina ambapo alikuwa akiishi Beit Hanina na kuomba hifadhi nchini Nicaragua na baada ya muda alianza maisha yake mapya katika jimbo la Michigan Marekani.
Rashida Tlaib alizaliwa Julai 24 mwaka 1976 Detroit nchini Marekani.
Ilhan alimshinda kwa kishindo mgombea mwenza Jenniffer Zilienski kwa asilimia zaidi ya 70.