Saleh awatumia salamu hizi Ndanda


Uongozi wa timu ya Yanga umesema kuwa maandalizi yapo vizuri kuhakikisha kwamba wanaendelea kuchukua pointi tatu muhimu katika michezo ambayo watacheza ikiwa ni pamoja na mchezo wa kesho dhidi ya Ndanda FC uwanja wa Taifa.

Mratibu wa Yanga Hafidhi Saleh amesema kuwa wana imani ya kufanya vizuri kutokana na kikosi ambacho wanacho pamoja na morali ya kupambana ili kuweza kupata matokeo.

Hafidhi alisema kuwa wamepambana kiasi kikubwa kutengeneza timu na kuweza kupata matokeo jambo ambalo linazidi kuwapa nguvu ya kusonga mbele.

"Ligi ni ngumu kwa kuwa kila timu imejipanga kupata matokeo ila hilo nalo halityupi shinda kwani lazima kuwe na ushindani ili kupata mshindi hivyo tupo tayari kwa ajili ya hilo.

"Mchezo wetu dhidi ya Ndanda tunajua utakuwa mgumu ila tunajua kwamba wachezaji wana morali na kuhakikisha wanashinda hivyo wataingia uwanjani kwa nidhamu ili kupata matokeo ambayo wanayahiaji." alisema.

Yanga wamefanikiwa kucheza michezo 9 na kushinda michezo 8 huku wakitoa  sare mchezo mmoja bila kupoteza hata mmoja, na mpaka sasa wakiwa wameweka kibindoni pointi 25 na kushika nafasi ya pili kwenye msimamo huku vinara wakiwa ni Azam wenye na pointi 27.