Simba yabanwa na Wamalawi

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara Simba SC, wameambulia sare ya bila mabao dhidi ya wageni wake, Nyassa Bullets kutoka Malawi.

Katika mechi hiyo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Simba walipoteza nafasi kadhaa za wazi.

Hata hivyo, wakati mwingine kipa, Deogratius Munish ‘Dida’, alilazimika kufanya kazi ya ziada kuzuia michomo ya wachezaji wa Bullets ambao walionyesha ni hatari.

Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems aliamua wachezaji wake wapate mechi za kujipima nguvu hasa kwa wale ambao hawajaitwa katika timu zao za taifa.

Simba ilionyesha kiwango kizuri katika mechi hiyo lakini tatizo la umaliziaji likaonekana kuiandama.