Simba yatangaza wachezaji wapya watakao wasajili dirisha dogo


Wakati kikosi cha Simba kikiwa katika maandalizi ya kuanza safari yake kuelekea Ligi Mabingwa Afrika dhidi ya Mbabane Swallows, imeelezwa wachezaji kadhaa watapelekwa kwa mkopo mahala pengine.

Taarifa imesema kwa mujibu wa aliyekuwa Kaimu Rais na sasa Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi, Salim Abdallah 'Try Again' amesema kuwa zoezi la kupokea ripoti ya watakaoondoka inasubiriwa kutoka kwa Kocha Mkuu, Patrick Aussems.

Abdallah ameeleza kuwa mpaka sasa bado Aussems hajafikisha ripoti hiyo hivyo usajili hauwezi ukafanyika bila kuipata kutoka kwake.

Licha ya ripoti kutowafikia, inaelezwa wachezaji Marcel Kaheza, Rashidi Mohammed na Said Mohammed ndiyo wanaopewa nafasi ya kupelekwa kwa mkopo kwenda timu zingine.

Abdallah ameeleza tayari timu kadhaa zimeshawasilisha ripoti ya kuwahitaji japo wao wametoa sharti la wachezaji wao kucheza kikosi cha kwanza.

Na kuhusisna na wale ambao Simba itawasajili, wanaotajwa mpaka sasa ni Ephrem Guikan kutoka Gor Mahia, pamoja na Francis Kahata ambaye anacheza klabu hiyo.

Aidha, kuna jina jingine kutoka KCCA ya Uganda ambalo halijawekwa wazi lipo kwenye orodha ya wachezaji ambao wanatajwa kusajiliwa na Simba pia.