https://monetag.com/?ref_id=TTIb Treni inayokwenda kwa kasi zaidi Afrika yazinduliwa Morocco | Muungwana BLOG

Treni inayokwenda kwa kasi zaidi Afrika yazinduliwa Morocco

 Morocco imezindua treni inayokwenda kwa kasi zaidi barani Afrika - itakayopunguza nusu ya muda unaotumika kusafiri katika miji ya kibiashara na kiviwanda Casablanca na Tangi

Mfalme Mohammed VI na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron waliipanda treni hiyo katika safari ya uzinduzi kutoka Tangier hadi katika mji mkuu Rabat.


Takwimu kuu kuhusu treni ya kasi Afrika:

  • Treni imepangiwa kwenda kwa kasi ya 320km kwa saa
  • Itakapunguza kwa zaidi ya nusu muda unaotumika kusafiri 200km kutoka mji wa Casablanca hadi Tangi kuwa safari ya saa mbili.
  • Inakwenda kwa kasi ya mara mbili zaidi kuliko treni ya mwendo kasi ya Afrika kusini inayouunganisha uwanja wa kimataifa wa ndege Johannesburg hadi katika mji wa kibiashara wa Sandton
  • Inagharimu 22.9 billion dirhams ($2.4bn; £1.8bn), kwa mujibu wa shirika la habari la kitaifa MAP
  • Ilichukua miaka saba kuijenga reli ya treni hiyo.


Afrika inatazamia kuimarisha miundo mbinu ya usafiri kushinikiza biashara, uwiano na utangamano wa kieneo.

Mataifa ya Afrika yanakumbatia mfumo wa reli ya mwendo kasi katika kujaribu kushinikiza na kukuza uchumi na kuimarisha kasi za kusafirisha bidhaa baina ya mataifa kibiashara.