https://monetag.com/?ref_id=TTIb VAR kutumika hatua ya mtoano Ligi ya Mabingwa msimu huu | Muungwana BLOG

VAR kutumika hatua ya mtoano Ligi ya Mabingwa msimu huu

Mfumo wa Msaidizi wa Video (VAR) unaweza kutambulishwa kwa haraka katika hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa ya msimu huu, UEFA ikisema imeamua kufanya uamuzi mwezi ujao.

Shirikisho hilo linaloongoza soka barani Ulaya lilisema mnamo Septemba kuwa VAR itaanzishwa kuanzia msimu wa 2019/20, lakini majadiliano yameendelea kwa wiki kadhaa za hivi karibuni, majadiliano yanayoonesha nia ya kutambulishwa haraka zaidi mfumo huo tofauti na ilivyotegemewa.

Kulingana na taarifa ya BBC, hofu ya UEFA kutokana na makosa ya waamuzi katika michezo mbalimbali na mafanikio ya VAR katika Kombe la Dunia mwaka huu, ni moja ya vishawishi vikubwa kwa viongozi hao kufikiria upya suala la kutambulisha teknolojia hiyo.

Mjadala kuhusu VAR umeshika kasi hivi sasa baada ya Manchester City kupewa penalti katika mchezo wa klabu bingwa Ulaya Jumatano ya wiki hii dhidi ya Shaktar Donetsk baada ya Raheem Sterling kujikwaa chini wakati akiwa na lengo la kufunga bao.

Mafunzo na warsha kwa waamuzi yanaendelea Ulaya nzima hivi sasa,  lakini UEFA inaamini kwamba sasa kuna viongozi wa kutosha barani humo  ambao wanafahamu vizuri VAR baada ya kuanzishwa miaka 16 iliyopita.

Ligi Kuu ya soka nchini Uingereza EPL ndiyo ligi pekee kati ya ligi 'tano kubwa' za Ulaya ambayo bado haijaanza kutumia teknolojia hiyo. Bundesliga na Serie A ziliiingiza teknolojia hiyo kabla ya msimu wa 2017/18, na Ligue 1 na La Liga zilianza kutumia miezi 12 baadaye.