Wajasiriamali nchini kunufaika na urasimishaji biashara



Wajasiriamali Nchini  kuendelea kunufaika na Mpango wa Kurasimisha Biashara katika mwaka wa fedha 2018/2019 ikiwa ni moja ya hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuwaniunua wajasiriamali hao.

Akizungumza wakati wa mafunzo kwa Wajasiriamali wa Halmashuri ya  Mji wa Njombe yanayolenga kuwajengea uwezo wajasiriamali ili waweze kurasimisha biashara zao na hivyo kuongeza tija na kuchangia katika ujenzi wa Taifa, Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania ( MKURABITA), Bi. Seraphia Mgembe amesema kuwa lengo ni kuwajengea uwezo  ili waweze kurasimisha  Biashara zao.

“Tunashukuru Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe Rais, Dkt. John  Pombe  Magufuli pamoja na Bunge kwa kuiwezesha MKURABITA kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi hasa katika eneo la kuwasaidia wajasiriamali wadogo ili warasimishe Biashara zao;’’ Alisisitiza  Mgembe.

Sehemu ya Wajasiriamali wa Halmashuri ya Mji wa Njombe wakimsikiliza Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha Biashara na Rasilimali za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) Bi. Seraphia  Mghembe (Hayupo pichani)  leo mjini Njombe wakati wa mafunzo kwa wajasiriamali wa  Halmashauri hiyo yanayolenga kuwajengea uwezo wa kurasimisha Biashara zao.

Akifafanua amesema kuwa mafunzo yakuwajengea uwezo Wajasiriamali hao yameendeshwa kwa siku 10 ambapo kila kundi lilikuwa na siku mbili za kujifunza mada mbalimbali zilizotolewa na wataalamu kutoka Taasisi mbalimbali zikiwemo benki  kama; CRDB Bank na  NMB .

Taasisi nyingine zilizoshiriki katika kutoa mada katika mafunzo hayo ni pamoja  na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo SIDO, Mamalaka ya Mapato nchini (TRA), Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) pamoja na wataalamu wengine wa ujasiriamali.

Pia, alipongeza ushirikiano ulipo kati ya MKURABITA na Mkoa wa Njombe hali iliyosaidia katika kufanisha mafunzo kwa wajasiriamali na pia urasimishaji ardhi kwa wananchi ambapo  baadhi yao wameweza kupata mikopo katika Taasisi za fedha na hivyo kuinua uchumi wao kutokana na kukua kwa shughuli za ujasiriamali walizokuwa wanafanya na hasa kutokana na mikopo waliyopata kutoka katika Taasisi za fedha zikiwemo Benki.

Afisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania  (TRA) Mkoa wa Njombe Bw. Stanley Sulle Akiwasilisha mada kwa wajasiriamali hao kuhusu taratibu za ulipaji kodi wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo ili waweze kurasimishaji biashara zao na hivyo kushiriki katika ujenzi wa Taifa kwa kulipa kodi, Mafunzo hayo yameandaliwa na MKURABITA.

Taasisi nyingine zilizowawezesha wajasiriamali kupata mikopo baada ya kurasimisha biashara zao ni pamoja na SIDO ambayo imekuwa ikiwajengea uwezo wajasiriamali waliojikita katika usindikaji wa bidhaa za mbogamboga na matunda ili kuongeza thamani na hivyo kuchochea ujenzi wa uchumi wa Viwanda katika Mkoa wa Njombe ambao unazalisha matunda ya aiana mbalimbali yakiwemo maparachi.

Mafunzo yakuwajengea uwezo wajasiriamali hao wa Halmashuri ya Mji wa Njombe ili waweze kwenda na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano inasisistiza ujenzi wa uchumi wa Viwanda.

Kwa upande wake Afisa kutoka mfuko wa NSSF Bw. Celestine Michael amesema kuwa kuna kila sababu ya kuendelea kuimarisha huduma zote zinazotolewa kwa wananchi. ni kuona kuwa matokea tarajiwa yanafikiwa kwa maslahi ya wananchi.

Baada ya urasimishaji wananchi wote wmetakiwa kutumia fursa za jambo hilo katika kukuza uchumi na Ustawi wa wananchi.

Aidha, Aliwaaasa  Wajasiriamali kutumia Kituo cha Huduma kwa Pamoja (One Stop Centre) kurasimisha Biashara zao ili kuchochea maendeleo na ustawi wajamii.

Akizungumzia hatua ya kuanzishwa kwa kituo hicho Bw. Michael amesema kuwa ni hatua kubwa katika kuwawezesha wajasiriamali kwani wataweza kurasimisha Biashara zao hali itakayowaongezea wigo wa kufanya ujasiriamali na kukuza masoko.

“Tunapongeza juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano kupitia MKURABITA kwani uwezeshaji wananchi kurasimisha biashara zao ni hatua kubwa katika kuchochea uchumi wa Viwanda na ujasiriamali kwa ujumla,” Alisisitiza Michael.