https://monetag.com/?ref_id=TTIb Wakulima wa vyama vya msingi 15 Nachingwea kuanza kusoma miamala ya fedha | Muungwana BLOG

Wakulima wa vyama vya msingi 15 Nachingwea kuanza kusoma miamala ya fedha




Na.Ahmad Mmow,Nachingwea.

VYAMA 15 vya msingi vya ushirika wilayani Nachingwea mkoa wa Lindi,tayari vimefanyiwa uhakiki ambao utawezesha wakulima wa korosho kuanza kulipwa.

Ayo yameelezwa leo na mkuu wa wilaya hiyo,Rukia Muwango alipozungumza na Muungwana Blog katika mamlaka ya mji mdogo wa Nachingwea.Mara baada ya kukagua maendeleo ya usafirishaji zao hilo katika maghala ya Lindi farmers.

Mkuu huyo wa wilaya alisema kati ya vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS)38, vilivyopo wilayani humu,tayari vyama 15 vimefanyiwa uhakiki wa taarifa za wakulima wake waliopeleka korosho sokoni katika msimu huu wa 2018.

Alisema kutokana na kukamilika uhakiki huo,wakulima waliopeleka korosho zao kwenye vyama hivyo wataanza kulipwa.Huku uhakiki katika vyama vingine ukiendelea.

Mbali na hayo Muwango alisema kupitia uhakiki na ukaguzi uliofanywa na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hii katika vyama vya msingi vya ushirika vya Nambambo,Naipingo na Ukombozi,wamebaini kwamba baadhi ya watu waliopeleka korosho kwenye vyama hivyo sio wakulima na hawana mashamba.

Alisema baadhi ya watu hao waliopeleka korosho maghalani sio wakazi wa wilaya hii na hawana mashamba.Hivyo alionya kuwa watu hao hawatalipwa.Kwani inadhihirisha kwamba ni miongoni mwa walionunua zao hilo nje ya mfumo rasmi.

"Mtu ukimuuliza anasema yupo Mwanza,unamuuliza anakiasi gani cha korosho na shamba lake lipo eneo gani anaishia kukata simu,tutendelea nazoezi hili ili kuwabaini waliowadhulumu wakulima,"alisema Muwango.

Kwamujibu wa Muwango kazi ya kusafirisha korosho kutoka katika maghala ya Lindi farmers inaendelea vema na hakuna changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa zoezi hilo.