Watu 42 wafariki kufuatia kulipuka kwa mtungi wa gesi ndani ya basi

Watu 42 wafariki na wengine wajeruhiwa baada ya basi walilokuwemo kulipuka moto jana usiku Gwanda nchini Zimbabwe.

Msemaji wa  jeshi la Polisi  la usalama barabarani Gwanda amesema kuwa watu 42 ndio ambao wamefariki katika ajali hiyo ya moto iliotokea katika basi la abiria usiku wa Alkhamis.

Kulingana na taarifa zilizotolewa muda mchache baada ya ajali,  moto huo  huenda ulisabishwa na mtungi wa gesi uliolipuka.

Shirika la msalaba mwekundu la Zimbabwe  limerusha katika ukurasa wake wa Twitter picha ya ajali hiyo zikionesha  basi hilo lilivyoteketea kwa moto.