.

12/09/2018

Ajali ya helikopta Sudan yaua maafisa wa Serikali

Ajali ya helikopta mashariki mwa Sudan imemuua gavana wa ajimnboa na takatiana maafisa wengine wanne.

Ndege hiyo ililipuka na ikashika moto baada ya kugonga mlingoti wa mawasiliano wakati ilijaribu kutua eneo moja la mbali la jimbo la Al-Qadarif, walioshuhudia waliliambia shirika la AFP.

Hakuna sababu rasmi iliyotolewa ya ajali hiyo.

Watu kadhaa walipelekwa hospitalini kutibiwa, vyombo va habari vilisema bila ya kutoa taarifa zaidi.

Kati ya wale waliouawa ni Al-Qadarif gavana wa Mirghani Saleh, mkuu wa baraza lake la mawaziri, mkuu wa polisi eneo hilo na waziri wake wa kilimo.

Ndege za jeshi la Sudan zilinunuliwa kutoka uliokuwa Muungano wa Usovieti.

Watu 8 walijeruhiwa mwezi Oktoba wakati ndenge mbili ziligongana kwenye uwanja wa ndege mjini Khartoum.

Mwezi Septemba, marubani wawili waliuawa wakati ndege ya jeshi ilainguka karibu na Omdurman huko Khartoum.