.

12/09/2018

Ally Kiba aanza vizuri Coastal Union

Kikosi cha Coastal Union, kinachonolewa na kocha Juma Mgunda kimekubali sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Mbeya City, katika mchezo wa Ligi kuu uliochezwa katika uwanja wa Mkwakwani Tanga.

Safu ya ushambuliaji ya Coastal Union iliyo chini ya Ally Kiba imefanikiwa kuandika bao mapema dakika ya 5 baada ya Kiba kusababisha kona ambayo ilipigwa na Athumani Idd 'Chuji'.

Mchezo wa leo umetawaliwa na ubabe kutokana na kila timu kuhitaji ushindi ili kujiweka kwenye nafasi nzuri kwenye Ligi.

Kipindi cha pili Bakari Mwanyeto alijifunga wakati akiokoa mpira katika eneo la hatari.