Chiddi Mapenzi afunguka kuachana na Shamsa Ford


Mfanyabiashara maarufu, Chiddi Mapenzi amefunguka kuhusu kuachana na mke wake ambaye ni msanii wa filamu, Shamsa Ford.

Chiddi kwenye Friday Night Live ya EATV amesema kuwa msanii huyo bado ni mke wake na hajaamua kumpost kwasababu yuko busy kwasababu anatarajia kufungua duka lake mwezi ujao.

"Shamsa ni mke wangu sio kwamba hapost, labda mwenyewe kaamua ana mambo yake lakini by the way anafungua duka lake soon mwezi ujao la kike kwahiyo hakuna tatizo lolote la kike nipo nae mama," amesema Chiddi Mapenzi.

"Unajua watu wengine wamezoea kupostiana sasa mimi siko hivyo wewe unanijua ndugu yangu, mimi mtu mzima siko hivyo mimi niko nae sema nilikuwa sipo nilikuwa safari juzi kati tu, kwahiyo mama niko nae sema yuko busy anataka kufungua ofisi yake anashinda dukani kwake."