Loading...

12/03/2018

Hawa ndio Wachezaji wa Simba ambao wataukosa mchezo wa Mbabane Kesho


Kesho Simba watakuwa kibaruani kurudiana na timu ya Mbabane Swallows nchini Eswatini  ukiwa ni mchezo wa ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ule wa awali uliochezwa uwanja wa Taifa, Simba kuibuka na ushindi wa mabao 4-1.

Jumla ya wachezaji 21 wapo Eswatini wakiwa chini ya kocha Patrick Aussems huku taarifa zikieleza kuwa beki mpya raia wa Burkina Faso, Zana Coulibary amewekwa pembeni na kocha mkuu.

"Yule beki mpya Coulibaly yeye hajaenda na timu kwa sababu kocha kapendekeza abaki Dar ili aendelee kujifua kwa sababu hakuwa na siku nyingi tangu amejiunga na wenzake katika mazoezi.

"Wachezaji wengine ambao hawajasafiri na timu ni pamoja na Marcel Kaheza, Asante Kwasi, Ally Salim hawa wamebaki Dar," kilieleza chanzo.


Loading...