Jibu la Petit baada ya kuachana na Esma Platnumz



Aliyekuwa mume wa Dada wa msanii Diamond Platnumz, Petit Man Wakuache amesema kuwa hana ugomvi na familia ya kina Esma Platnumz baada ya kuachana na ndugu yao.

Petit amesema kuwa  kuchanika kwa jamvi sio mwisho wa maongezi na ndio mama yeye na mkwe wake bado wanaongea vizuri bila tatizo.

"Sina ugomvi wowote na familia ile, ndio maana hadi leo unaona mimi na mama tunaongea vizuri tunakomentiana vizuri kuchanika kwa jamvi sio mwisho wa maongezi," Patit ameiambia Dizzim Online.

Hata hivyo Petit kasema kuwa kwasasa yupo kwenye mahusiano mengine.