.

12/06/2018

Jibu la Shetta kuhusu wimbo wake kufanana na wa NandyMsanii wa Muziki, Shetta amefunguka wimbo wake mpya wa 'Hatufanani' beat yake kufanana na wimbo wa Nandy wa 'Aibu'.

Shetta akiwa Times FM amesema kuwa alipousikia wimbo wa msanii huyo alilipenda beat hivyo akamuomba Producer Kimambo na Nady autumie na wao wakamkubalia.

Licha ya hivyo, Msanii huyo amesema kuwa alipata comment kwa watu wasio na uelewa walimshambulia wakidai amemkopi msanii mwenzake huku akisema kuwa awali aliwaza kufanya 'Aibu' remix.