Jinsi ya kulinda afya ya moyo ili usipatwe na magonjwa



Miongoni mwa magonjwa yanayotawala sehemu kubwa ulimwenguni kote ni magonjwa ya moyo, pamoja na kuwako na takwimu hiyo, zifutazo ndizo mbinu za kuulinda moyo ili usipatwe na magonjwa ya moyo.

Hakikisha unatumia kwa wingi vyakula vyenye nyuzinyuzi au fiber kwa wingi, jamii za maharage, mboga za majani, karanga, na matunda ni vyanzo vizuri vya kambakamba.

Epuka kabisa vinywaji na vyakula vilivyosindika kama soda, juisi, enegy drink maana ni chanzo kikubwa cha watu kuugua kisukari, uzito mkubwa na kitambi na magonjwa ya Moyo.

Ongeza matumizi ya mafuta ya omega 3 ama ukatumia virutubisho vyenye mafuta haya kwani husaidia kulainisha mishipa ya damu na kuzuia kuganda kwa damu wakati wa usafirishaji.

Epuka matumizi ya pombe kwani huongeza kiwango cha mafuta mabaya kwenye mishipa ya damu (triglycerides), na pia kuongeza mafuta kwenye ini na hatimae ini kufeli kufanya kazi.

Jiwekee ratiba ya kufanya mazoezi walau mara 3 kwa week, inasaidia kutoa sumu kwenye mwili na kurekebisha presha yako ya damu.