Kim Kardashian aingilia kati ugomvi wa Kanye West na Drake

 Baada ya sakata kati ya Kanye West na Drake kuendelea usiku wa kuamkia jana December 14,2018 kupitia ukurasa wa Twitter wa Kanye, Kim Kardashian hakutaka mumewe kupewa vitisho na hivyo kuingilia kati ugomvi huo.

Kim Kardashian ametumia page take ya twitter kumuonya Drake kuacha kumtishia maisha Mume wake kwasababu jina la Drake limetokana na Kanye West kumtengenezea njia ya yeye kujulikana, tamko hili limekuja baada ya Kanye kudai kuwa Drake amekuwa akimpigia simu na kumpa vitisho.

Baada ya Kim Kardashian kumkingia kifua mume wake alitweet ujumbe mwingine na kusema kuwa mumewe ni mwenye akili nyingi amevunja rekodi kutoboa mipaka mingi sana kila kitu kwenye muziki, ubunifu wa jukwaani, mitindo na utamaduni na ataendelea kuibadilisha dunia.