.

12/09/2018

KMC yaipiga mkwara mzito Azam FC

Timu ya KMC, iliyo chini ya kocha mkuu Etiene Ndiragije imewatangazia vita kali wapinzani wao Azam FC watakaokutana nao kesho uwanja wa Uhuru.

Azam FC watakuwa wageni kwa KMC kesho uwanja wa Uhuru wakiwa na kumbukumbu ya kupata matokeo mazuri katika mchezo wao wa mwisho dhidi ya Mbao, ila KMC wamesema wamejipanga.

Ofisa habari wa KMC, Anwar Binde amesema maandalizi yamekamilika kwa asilimia kubwa kilichobaki ni vitendo uwanjani.

"Wachezaji wapo tayari baada ya kurejea kutoka kanda ya ziwa sasa ni zamu yetu kuutumia vizuri uwanja wa nyumbani kupata pointi tatu," alisema.

KMC wamepoteza michezo 3 kati ya 14 waliyocheza watakutana na Azam FC ambayo haijapoteza mchezo kati ya 15 waliyocheza mpaka sasa.