https://monetag.com/?ref_id=TTIb Martin kutemwa Yanga sababu hizi hapa | Muungwana BLOG

Martin kutemwa Yanga sababu hizi hapa

SIKU moja baada ya mshambuliaji wa Yanga, Emmanuel Martin kutajwa kujiunga na klabu ya Ruvu Shooting, imeleezwa sababu ya kutoongezewa mkataba mpya kumetokana na mchezaji kutomshawishi kocha wake Mwinyi Zahera uwanjani.

Zahera, ajavutiwa na kiwango cha mchezaji huyo wa zamani wa JKU ya Zanzibar na kushauri kutoongezewa mkataba mpya baada ya ule wa kwanza kumalizika tangu Novemba mwaka huu.

Martin sasa amejiunga na Ruvu Shooting ikiwa ni siku mbili kabla ya dirisha dogo la usajili alijafungwa.

Dirisha hilo la usajili lilifunguliwa Novemba 15 na litafungwa leo usiku (5:59).

Mmoja wa viongozi wa klabu hiyo alisema kuwa awali kamati ya usajili ilipanga kumuongezea mkataba mshambuliaji huyo na walikuwa wakisubiri maamuzi ya kocha wao.

“Lakini Kocha alishauri kutomuongezea mkataba, na kama kamati inasikiliza na kufuata ushauri wa kocha,” alisema kiongozi huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe.

Martin aliyesaini mkataba wa mwaka mmoja kuichezea Ruvu Shooting, alijiunga na Yanga kwenye msimu wa mwaka 2016/2017