Mhandisi atiwa mbaroni kwa kuomba rushwa ya ngono

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) jijini Dar inamshikilia Mhandisi wa Kampuni ya Mask and Sons, Leonard Mkaka kwa tuhuma za kuomba rushwa ya ngono

TAKUKURU ilimuwekea mtego katika nyumba ya kulala Wageni ya Nara Beach Lodge iliyoko Kigamboni na kufanikiwa kumkamata

Kampuni anayofanyia kazi imepewa zabuni ya kutengeneza barabara katika Halmashauri ya Temeke maeneo ya Toangoma mtaa wa Masaki jijini humo

Anaelezwa kuvunja kifungu cha 25 cha sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11/2017 na atafikishwa Mahakamani kufunguliwa mashtaka