Mzee atumia mwaka mmoja kuiona njia kwenda kumfuata mtoto wake kwa wachawi



Na James Timber, Mwanza

Mzee Idrisa Hussein Mkazi wa  Igombe Kata ya Bugogwa katika Wilaya ya Ilemela jijini Mwanza amesaidiwa na Mganga kutoka Ufipa kwa kumuonesha njia ili kumfuata mwanaye aliyekuwa amepotezwa kimazingara  kwa zaidi ya kipindi cha mwaka mmoja na nusu.

Baba wa mtoto huyo amesema kuwa aliamua kuchukua maamuzi ya kuwatafuta wataalamu kutoka Ufipa kutokana na kuzunguka kwa wanganga zaidi ya nane lakini uganga wao kushindwa kufanikisha kupatikana kwa mtoto huyo.

Aidha ameongeza kuwa jambo lililochangia aamini kuwa mwanaye alichukuliwa kwa njia za kishirikina ni baada ya kuiona mara kwa mara taswira ya  picha ya mwanaye usoni.