Sauti Sol wathibitisha kufanya kolabo na Harmonize


Kundi la Muziki la Sauti Sol kutoka nchini Kenya wamethibitisha kufanya kolabo la Harmonize.

Sauti Sol wamesema kuwa tayari msanii huyo alivyokuja Nairobi wakampigia wakaingia studio kwasasa kilichobaki ni kufanya video.

"Harmonize ni rafiki yetu alikuwa amekuja Nairobi akatupigia tulikua tukiambia kuwa tutafanya nyimbo all the time lakini hatukupata nafasi, this time alitupigia tulikuwa area tukampigia tuaingia studio akaua verse sasa hivi tunataka kushoot video kati ya huu mwaka au next year," Wamesema Sauti Sol walipowasili nchini.