.

12/09/2018

Simba wapata mbinu ya kuiangamiza Nkana FC


Mshambuliaji wa timu ya Simba, Meddie Kagere raia wa Rwanda amesema kikubwa kitakachowapa matokeo kwenye mchezo wa hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika ni ushirikiano na juhudi.

Kagere mwenye mabao 2 kimataifa, aliwafunga Mbabane Swallows ya Eswatini, atakuwa miongoni mwa msafara utakaoifuata Nkana FC  ya Zambia.

"Tumepita hatua ya awali baada ya kushinda na hicho ndicho tutakachofanya ili kufika katika hatua inayofuata, tumejiandaa kufanya vizuri katika michezo yetu yote.

"Tunaamini kwamba tunaweza kupata matokeo kwa ushirikiano tukiwa ni timu pia kwa juhudi binafsi na uwezo wa kujiamini ni vitu vya msingi na tutafanya makubwa kwa sasa," alisema.

Simba watacheza na Nkana FC katika mchezo wa hatua ya kwanza dhidi ya Nkana FC ya Zambia Desemba 14 nchini Zambia na mchezo wa marudio unatarajiwa kuchezwa Dar es Salaam Desemba 21.