SMZ yawafunda wasimamizi wa sheria na haki kuhusu kutokomeza dawa za kulevya


Na. Thabit Madai, Zanzibar.

Waziri wa nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar, Mohammed Aboud Mohammed amevitaka vyombo vya usimamizi wa sheria na haki nchini kufanya kazi kwa mashirikiano ili kuhakikisha wanabuni mbinu imara zitakazo saidia katika kupambana na biashara haramu ya dawa za kulevya.

Alisema kufanya kazi kwa mashirikiano kwa vyombo hivyo  kutasaidia kwa kiasi kikubwa katika mapambano dhidi ya  biashara hizo haramu pamoja na  kuinusuru jamii kwa matumizi ya dawa za kulevya  ambazo zimekuwa zikirudisha nyuma maendeleo ya Taifa.

“Njia pekee ya kupambana na dawa za kulevya ni kushirikiana na kusimama imara kwa Taasisi zote zinazosimamia sheria na haki kama vile jeshi la Polisi, majaji, mahakimu muendesha mashtaka pamoja na wanasheria  kwa kuhakikisha kuwa  wanatekeleza majukumu yao ya kazi kwa kuzingatia Maadili, uweledi wa kazi na kuweka mbele maslahi ya taifa” alisema Mohammed aboud Mohameed.

Wito huo ameutoa wakati akifungua warsha ya siku mbili kwa Majaji, Mahakimu, Maofisa wakuu wa polisi wa idara ya upelelezi, wanasheria wa serikali pamoja na mkurugenziwa Mashtaka, ambapo Warsha hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abduliwakili kikwajuni Mjini Magharib Unguja.

Aidha  Mhe, Aboud Alisema Dawa za kulevya ni janga la taifa ambalo linaathiri kwa kiasi kukubwa nguvu kazi na uchumi wa taifa.

“kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na Dawa za kulevya na uhalifu duniani (UNODC-2015) Zanzibar inakisiwa na wastani wa watumiaji 10000 ya dawa za kulevya kati hao 3200 wanatumia kwa kujidunga” alieleza Mhe, Mohammed Aboud.

Aliendeea kueleza kuwa  kuwa watumiaji hao wa dawa za kulevya wameathirika lvirusi vya ukimwi na homa ya ini  ya B na , kifua kikuu pamoja na maradhi ya ngozi.

Hata hivyo alisema  kueleza kuwa Takwimu hizo ni kiashiria kuwa cha hatari kwa nchi yenye Idadi ndogo ya watu inavyoweza kuathiri malengo ya Serikali katika kufikia Dira ya maendeleo ya 2020 ya zanziba.

Aidha aliwata wasimamizi hao wa sheria na hai kutumia warsha hiyo katika kuimarisha mawasiliano kwa kuhakikisha sheria ya udhibiti wa dawa za kulevya inatekelzwa kwa usahihi ili kuweza kufikia lengo la serikali ya zanzibar katika kuondoa kabisa dawa za kulevya.

Nae Mkurugenzi wa Mtendaji Tume ya kuratibu na kudhibiti Dawa za kulevya Zanzibar Heriyangu Mgeni khamisi   alisema  kwa hivi sasa hali ipo vizuri kwani Taasisi zote za hili sugu kwa Taifa.

“Kufanya kazi kwetu kwa mashirikiano kunapelekea kuwabaini wahusika wakubwa biashara hizi ambapo kwa mwaka 2017 hadi 2018 tumewakamata wahusika 15 ambao kwa sasa wameshafikishwa sehemu husika na kuchukuliwa kwa hatua za kisheria” alisema Heriyangu mgeni khamis.

Warsha hiyo ya siku mbili imewahusisha Majaji, Mahakimu,Jeshi la Polisi ,wanasheria wa serikali pamoja na Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar kwa lengo la kujadili mambo mbali mbali.