Vyama vya ushirika vyashauriwa kuanzisha miradi ya kiuchumi.Na.Ahmad Mmow,Nachingwea.

VYAMA vya ushirika nchini vimeshauriwa kuanzisha miradi ya kiuchumi ili viweze kupata mafanikio na kufikia maendeleo yaliyokusudiwa wakati vinaanzishwa.

Wito huo umetolewa leo na kaimu mrajisi wa tume ya maendeleo ya ushirika,Tito Haule wakati wa hafla ya kuwekwa jiwe la msingi la ofisi kuu ya chama kikuu cha ushirika cha RUNALI,iliyofanyika katika mamlaka ya mji mdogo wa Nachingwea.

Haule ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye hafla hiyo  alisema vyama vya ushirika vinakilasababu ya kuanzisha miradi ya kiuchumi li viweze kutimiza dhamira ya kuanzishwa kwake.Hasa kujiletea maendeleo kwa faida ya wanachama wake,ambao ni wakulima.

 Alisema katika uanzishaji wa miradi ya uchumi,vyama havinabudi kufikiria namna bora ya kuwekeza ili viendelee na kusonga mbele kimaendeleo  badala ya kutegemea vyanzo vichache.Ikiwamo ushuru unaotokana na mauzo ya mazao.

Kaimu mrajisi huyo wa tume ya maendeleo ya ushirika nchini alibainisha kwamba licha ya kuanzizha miradi ya uchumi lakini pia viwekeze kwa kuzingatia mnyororo wa thamani.Ambapo kwa kanda hii ya kusini mnyororo wa thamani upo kwenye zao la korosho.

Alisema vyama vinaweza kuwekeza katika maeneo mengine ya kijamii.Hata hivyo kuwekeza kwenye mnyororo wa thamani kunaweza kurahisisha mambo mengi na kuongeza kasi ya mafanikio ya kufikia maendeleo ya vyama hivyo.

"Sasa hivi tunahangaika na habari za maghala ya kuhifadhia mazao,kama tungewekeza kwenye maghala tusingeteseka.Tunahangaika na usafirishaji,tungewekuwa na magari tusingehangaika na kuteseka kama hivi," alisema Haule.

Kama hiyo haikutosha,Haule aliendelea kuvielimisha vyama vya ushirika njia bora na zenye tija katika uwekezaji,kwa kusema vyama hivyo vifikirie kuanzisha viwanda ili viongeze thamani ya mazao ya wanachama wake ili yaweze kuuzwa na kununuliwa kwa bei nzuri.

Aidha Haule aliwageukia viongozi wa vyama vya ushirika kwakuwaambia wanatakiwa kuwa waadilifu na waaminifu.Kwani uaminifu na uadilifu ni nyenzo kuu ya uwazi na uwajibikaji ambao ni msingi wa utawala bora unaosababisha taasisi kupiga hatua kubwa ya maendeleo.

"Lakini viongozi lazima wawe na weledi,na huwezi kuwa na weledi bila kujua sheria,taratibu na kanuni.Kila chama cha msingi cha ushirika kinatakiwa kutenga asilimia kumi,ni sheria kwa ajili ya kuwapa wanachama wake elimu,mafunzo na habari," alisisitiza Haule.

Kwaupande wake mwenyekiti wa RUNALI,Hassan Mpako licha ya kuishukuru na kuipongeza serikali kwa kuamua kununua korosho na kumaliza sitofahamu ya ununuzi wa zao hilo katika msimu huu wa 2018/2019.Alitoa wito kwa serikali kusukuma na kuharakisha malipo ya wakulima wa korosho.

Aidha mwenyekiti huyo alitoa wito kwa serikali kuhusu nia njema ya serikali ya kuwatambua walionunua korosho nje mfumo rasmi.Alisema zoezi hilo lisiwe chanzo cha kuwaumiza wakulima kwa kuwcheleweshea malipo yao.Huku pia akiiomba serikali iharakishe malipo ya wasafirishaji na wachukuzi wa mizigo maghalani.

Chama kikuu cha ushirika Cha RUNALI,mbali na ujenzi wa ofisi hiyo ambayo gharama yake hadi kumalizika utamia shilingi 139.00 milioni.Lakini pia inatekeleza miradi mingine.Ikiwemo ujenzi wa ghala la kuhidhia mazao ambalo hadi kukamilika litatumia shilingi 1.37 bilioni.

Miradi mingine inayotekelezwa na chama hicho ambacho kilianzishwa mwaka mwaka 2013 nakupata usajili wa kudumu mwaka mwaka huu(2018) kwa namba za usajili 5597 ni ghala dogo na kituo cha malipo ya wakulima.